ZIARA YA KATIBU MKUU KIONGOZI MKOA WA ARUSHA KUKAGUA SHUGHULI ZA UTUMISHI WA UMMA KATIKA SEKRETARIETI YA MKOA WA ARUSHA SEPTEMBER 18,2014

 

IMG_5688

 

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. John Mongella, mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja, kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Bw. Jowika Kasunga, Septemba 18, 2014.

 

IMG_5709

 

 

 

 

 

 

 

 

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kushoto), akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Bw. Jowika Kasunga, Septemba 18, 2014.

IMG_5734

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (wa pili kushoto), akielekea kwenye Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha kukagua Mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya Kielektroniki (LGRCIS). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. John Mongella, kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Anza A. Ndossa na wa pili kulia nia Katibu Mkuu – TAMISEMI, Bw. Jumanne A. Sagini, Septemba 18, 2014.

IMG_5741

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. John Mongella na kushoto ni Katibu Mkuu – TAMISEMI, Bw. Jumanne A. Sagini, Septemba 18, 2014.

IMG_5789

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Bw. Juma R. Iddi, akitoa maelezo mafupi kwa Katibu Mkuu Kiongozi (hayupo pichani) jinsi Mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya (LGRCIS) unaotumiwa na Halmashauri hiyo katika kukusanya mapato yake unavyofanya kazi.

IMG_5808

Mkuu wa wilaya ya Arusha, Mhe. John Mongella (aliyesimama) akimshukuru Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (kushoto) kwa ujio wake na kukagua Mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya Kielektroniki (LGRCIS), katika Ofisi za Halmashuri ya Jiji la Arusha, Septemba 18, 2014. IMG_5818

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (wa nne kushoto waliosimama mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Septemba 18, 2014.

IMG_5828

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Dk. Frida Mokiti (kushoto), akimkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (kulia) hospitalini hapo ili kujionea Mfumo wa Kielektroniki wa ukusanyaji fedha za uchangiaji wa huduma za afya, Septemba 18, 2014.

IMG_5829

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa wasimamzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa ukusanyaji fedha za uchangiaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha, Septemba 18, 2014.

IMG_5858

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Anza A. Ndossa, akisoma taarifa ya kiutendaji ya Mkoa kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi kuzungumza na Menejimenti na Watumishi wa Halmashauri ya Mkoa wa Arusha na Halmashauri zake, Septemba 18, 2014.

IMG_5885

 

 

 

 

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, akizungumza na Menejimenti na Watumishi wa Halmashauri ya Mkoa wa Arusha na Halmashauri zake, katika kikao kilichofanyika katika Hoteli ya Naura Springs mjini Arusha, Septemba 18, 2014.       (hawapo pichani)

IMG_5925

Baadhi ya Watumishi wa Mkoa wa Arusha na Halmashauri zake, wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika katika Hoteli ya Naura Springs mjini Arusha, Septemba 18, 2014

IMG_5941

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (wa nne kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha mara baada ya mlkutano wake nao, uliofanyika katika Hoteli ya Naura Springs mjini Arusha, Septemba 18, 2014.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *