RAIS MHE.DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA AFYA WA KENYA KUHUSU TANZANIA KUPELEKA MADAKTARI 500(WASIO NA AJIRA SERIKALINI) KWENDA KUFANYA KAZI NCHINI KENYA MARCH 18,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu kuhusu Tanzania kupeleka madaktari 500 nchini Kenya, Ajira za Madaktari hao zitatangazwa mara moja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini(hawapo katika utumishi wa umma au taasisi za serikali) waliomaliza mafunzo kwa vitendo na ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari la Tanganyika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na ujumbe kutoka nchini Kenya uliongozwa na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam March18

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana wa Kisumu County Jack Rangumba ambaye aliambatana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu aliyeambatana pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu mara baada ya kumaliza mazungumzo yao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuelekeza jambo Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu pamoja na Gavana wa Kisumu County Jack Rangumba kabla hawajaondoka Ikulu jijini Dar es Salaam

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza kuhusu Kutangaza ajira za Madaktari wapatao 500 ambao watakwenda kufanya kazi nchini Kenya. Ajira hizo zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini(hawapo katika utumishi wa umma au taasisi za serikali. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *