RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA AWASILI CHATO KWA AJILI YA KUKABIDHI NYUMBA 50 ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA MIKOA YA SIMIYU, KAGERA NA GEITA JULAI 9,2017

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato Mkoani Geita. Rais Mstaafu Mkapaambapo julai 10,2017 anatarajiwa kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita. Balozi huyo wa Japan katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi mtambo wa kukamua Mafuta ya Alizeti (Double Refine) uliojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali ya Japan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa pamoja na wageni mbalimbali waliofika Chato kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazotarajiwa kufanyika kesho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Geita Josheph Kasheku Msukuma aliyefika Chato pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita. PICHA NA IKULU

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *