AIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU PAMOJA NA WAGONJWA WENGINE WALIOLAZWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JANUARI 6,2018

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyelazwa kwa ajili ya matibabu katika Wodi ya Mwaisela iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo amelazwa akipatiwa matibabu ya majeraha baada ya kujeruhiwa na Mbwa wake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfunika shuka Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngambale Mwiru alipomtembelea kumjulia hali katika Wodi ya Mwaisela hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ambapo amelazwa akipatiwa matibabu ya majeraha baada ya kujeruhiwa na Mbwa wake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Dkt.Ibrahim Mkoma anayemuhudumia Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngambale Mwiru ambaye amaelazwa katika Wodi ya Mwaisela hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ambapo akipatiwa matibabu ya majeraha baada ya kujeruhiwa na Mbwa wake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Kaka wa Profesa Anna Tibaijuka ajulikanaye kwa jina la Richard Kajumulo ambaye amelazwa katika Wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali na Profesa Anna Tibaijuka paomoja na mgonjwa ambaye ni kaka yake ajulikanaye kwa jina la Richard Kajumulo  aliyelazwa katika Wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimwagia maji ya Baraka Kaka wa Profesa Anna Tibaijuka ajulikanaye kwa jina la Richard Kajumulo ambaye amelazwa katika Wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Nasoro Rashid aliyelazwa katika Wodi ya ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mzee Hamadi Lila aliyekuwa akilia kwa furaha mara baada ya kumuona Rais alipofika katika wodi ya Sewahaji Jijini Dar es Salaam Januari 6,2017.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi kuhusu hali ya  watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimu Manesi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  mara baada ya kutembelea wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi pamoja na wafanyakazi wengine wa Taasisi hiyo mara baada ya kutembelea wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi mara baada ya kutembelea wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt.Khuzeima Khanbahi Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo anayewahudumia Mapacha walioungana Maria na Consolata  pamoja na Profesa Janabi mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete baada ya kuwa tembelea na kuwajulia hali hospitalini hapo Januari 6,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wapishi wanaofanya kazi ndani ya Hospitali ya Muhimbili wakati akitoka kuona wagonjwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *