RAIS WA ZIMBABWE MHE.EMMERSON MNANGAGWA AWASILI NCHINI NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI.JUNI 28,2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama akimsubiri mgeni wake Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa akiwasili nchini katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.Juni 28,2018.

Rais wa Zimbabwe Mhe.Emmerson Mnangagwa akiwasilli nchini katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.Juni 28,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama huku mgeni wake Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akimlaki mtoto baada ya kuakabihiwa Ua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya Rais huyo wa Zimbabwe kuwasili nchini.Juni 28,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikumbatiana  na mgeni wake Rais wa Zimbabwe Mhe.Emmerson Mnangagwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya Rais huyo wa Zimbabwe kuwasili nchini.Juni 28,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgeni wake Rais wa Zimbabwe Mhe.Emmerson Mnangagwa kwa Viongozi wa Ulinzi na Usalama mara baada ya Rais huyo wa Zimbabwe kuwasili nchini katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere .Juni 28,2018.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wakati nyimbo za mataifa mawili ya Tanzania na Zimbabwe zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya Rais huyo wa Zimbabwe kuwasili nchini.Juni 28,2018.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.Juni 28,2018.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akipunga mkono kwa wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya ziara ya kazi ya siku mbili.Juni 28,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.Juni 28,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wakifurahi wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.Juni 28,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha pamoja na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.Juni 28,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam.Juni 28,2018.

 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam.Juni 28,2018.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *