RAIS WA ZIMBABWE EMMERSON MNANGAGWA ATEMBELEA CHUO CHA KILIMO NA MIFUGO CHA KAOLE BAGAMOYO MKOANI PWANI AMBACHO MIAKA YA 1960s ILIKUWA SHULE YA MAFUNZO YA UFUNDI YA WAPIGANIA UHURU WA CHAMA CHA FRELIMO.JUNI 29,2018.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Edmund Mndolwa mara baada ya kuwasili katika chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani. Rais huyo wa Zimbabwe alisoma Shuleni hapo mwaka 1963 pamoja na wapigani Uhuru wa Chama cha FRELIMO na ilijulikana kama Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigania Uhuru wa Chama cha FRELIMO.Juni 29,2018.

 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza na wafanyakazi pamoja na wanafunzi wanaosoma katika Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole ambapo miaka ya nyuma alisoma hapo wakati huo ikijulikana kama Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO.Juni 29,2018.

 

 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiangalia moja ya sufuria waliokuwa wakiitumia katika matumizi yao ya kila siku wakati wakisoma katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO.Juni 29,2018.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiwa katika picha na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Edmund Mndolwa, Viongozi wengine wa Tanzania na Zimbabwe pamoja na wanafunzi wanaosoma katika chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati alipokuwa akielekea katika moja ya madarasa ambayo walikuwa wakiyatumia kuanzia mwaka 1963.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akitoka katika moja ya mabweni waliyoyatumia katika mwaka 1963 wakatika wakiwa katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO ambacho sasa kina julikana kama chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi mara baada ya kumaliza kukagua baadhi ya madarasa na mabweni waliyokuwa wakiyatumia katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO ambacho sasa kinajulikana kama chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akipunga mkono kwa kikundi cha ngoma za asili wakati akiondoka katika eneo la chuo hicho cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani.Juni 29,2018

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *