RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WAHUDHURIA MISA YA SHUKURANI YA UHAI YA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA KUTIMIZA UMRI WA MIAKA 80

Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimpa zawadi ya kadi na kisha kumpongeza Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa na mkewe Mama Anna Mkapa kwa kutimiza umri wa miaka 80 katika Misa ya Shukurani ya uhai iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam. Novemba 12, 2018

Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa pamoja na Maaskofu wakati wa Misa ya Shukrani kwa Mhe. Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam.Novemba 12, 2018

Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea kwa furaha na  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa baada ya  Misa ya Shukurani kwa  Mhe. Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata  jijini Dar es salaam.Novemba 12, 2018

Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Misa ya Shukurani ya  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam.Novemba 12, 2018.Kulia kwa Mhe. Mkapa ni mkewe Mama Anna Mkapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *