WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASSA AREJEA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM NA KUPOKEWA NA MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akiwasili katika Ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi CCM Lumumba jijini Dar es Salaam kabla ya kutangaza rasmi kurejea katika Chama cha Mapinduzi CCM. tarehe 1 Machi 2019.

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia. Wakwanza kushoto ni Kada wa CCM Rostam Azizi

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye ametangaza kurejea chama cha Mapinduzi CCM akitokea chama cha CHADEMA katika Ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi CCM Lumumba jijini Dar es Salaam

 

 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally wakizungumza jambo na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kurejea CCM akitokea CHADEMA.

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisalimiana kwa furaha na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia.

 

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akitangaza rasmi kurejea chama cha Mapinduzi CCM mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula, Katibu wa CCM Bashiru Ally, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamojan na Kada wa CCM Rostam Azizi.

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akitangaza rasmi kurejea chama cha Mapinduzi CCM mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula, Katibu wa CCM Bashiru Ally, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamojan na Kada wa CCM Rostam Azizi.

 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kumkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye amerejea rasmi CCM.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *