RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA TABORA-KOGA MPANDA KM 342.9, AFUNGUA BARABARA YA STALIKE MPANDA KM 36.9 PAMOJA NA STAND YA MABASI YA MIZENGO PINDA MPANDA MKOANI KATAVI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale wa kwanza kulia, Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe pamoja na viongozi wengine.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 katika sherehe fupi zilizofanyika katika manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri kuashiria ufunguzi wa barabara ya Stalike Mpanda km 36.9 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe fupi zilizofanyika katika manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi.

 

Sehemu ya Barabara ya Mpanda –Stalike iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe mara baada ya kuzindua na kufungua miradi ya barabara mkoani Katavi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakandarasi, Wahandisi Washauri wa miradi ya barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 katika sherehe fupi zilizofanyika katika manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi waliojikusanya pembezoni mwa barabara za Mpanda mjini mara baada ya kufungua miradi ya barabara mkoani Katavi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Stendi Kuu ya Mabasi Mizengo Pinda nje kidogo ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kufungua stendi hio ya mabasi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea nje ya lango kuu ya Stendi hio ya mabasi kuzungumza na wananchi mara baada ya kuifungua

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Azimio Mpanda mkoani Katavi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Mpanda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Azimio Mpanda mkoani Katavi kwa ajili ya kuwahutubia.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi kuwaaga mara baada ya kuhutubia katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Azimio Mpanda mkoani Katavi

Wanakwaya ya Agape wakitumbuiza katika uwanja wa Azimio Mpanda mkoani Katavi mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili uwanjani hapo.

Kwaya ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpanda Girls wakitumbuiza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili uwanjani hapo.

Kwaya ya Manispaa ya Sumbawanga ikitumbuiza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika uwanja wa Azimio mkoani Katavi. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *