Taarifa kwa vyombo vya Habari

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu, Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bi. Mariam Perla Mmbaga kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu.
Kabla ya uteuzi huo, Bi. Mariam Perla Mmbaga alikuwa Mkurugenzi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Bi. Mariam Perla Mmbaga anachukua nafasi ya Bw. Jumanne Sagini.
Bi. Mariam Perla Mmbaga ataapishwa Jumatatu tarehe 06 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *