Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia Mhindi wa Kuchoma alionunua kutoka kwa mfanyabiashara mdogo katika eneo la Dumila Darajani wakati akielekea mkoani Dodoma.
.Wafanyabiashara wa Dumila Darajani wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kusimama katika eneo hilo wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma. Rais amewaahidi kiasi Cha shilingi milioni mia moja za kujengea vibanda vizuri vya kufanyia biashara zao katika eneo hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wafanyabiashara huku ameshikilia Mhindi wa Kuchoma alioununua wakati akielekea mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono kuwaaga wafanyabiashara wadogo katika eneo la Dumila Darajani wakati akielekea mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Mhindi wa Kuchoma kutoka kwa mfanyabiashara mdogo katika eneo la Dumila Darajani wakati akielekea mkoani Dodoma.