RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ARUDISHA FOMU ZA MAOMBI YA KUGOMBEA URAIS KATIKA UCHAGUZI MKUU 2020 KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KATIKA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA NEC JIJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akirudisha Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 25 Agosti, 2020.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage pamoja na Mkurugenzi wa NEC Dkt. Wilson Charles wakihakiki Fomu za Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 25 Agosti, 2020.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage (aliyesimama) akitangaza kumteua Mgombea wa kiti cha (Urais) Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kurejesha fomu za uteuzi kwenye ofisi za Tume zilizopo Njedengwa jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa Fomu zake na kuzihakiki mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 25 Agosti, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 25 Agosti, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Wafanyakazi wa NEC mara baada ya kurejesha Fomu na kuteuliwa kuwa Mgombea kupitia Tiketi ya CCM Njedengwa jijini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC jijini Dodoma kwa ajili ya kurejesha Fomu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 25 Agosti, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mgombea Mwenza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakipokea Seti moja ya Fomu ya Uteuzi 8A, Fomu namba 10 pamoja na Picha za Wagombea kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 25 Agosti, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC jijini Dodoma mara baada  ya kurejesha Fomu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiwaaga viongozi wa chama waliofika katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC jijini Dodoma kushuhudia zoezi la kurejesha Fomu.

PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO LA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIRUDISHA FOMU ZA MAOMBI YA KUGOMBEA URAIS KATIKA UCHAGUZI MKUU 2020 KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KATIKA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA NEC JIJINI DODOMA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *