Waziri wa TAMISEMI Mhe.Hawa Ghasia na naibu wake Mhe. Aggrey Mwanri wakimkaribisha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya St.Gaspar mjini Dodoma Machi 17,2015 kwa ajili ya kufungua rasmi mafunzo ya wakuu wa wilaya wapya yanayofanyika katika ukumbi wa hoteli hiyo
Waziri wa TAMISEMI Mhe.Hawa Ghasia akitoa hotuba ya utangulizi kwa ajili ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipowasili katika Ukumbi wa Hoteli ya St.Gaspar mjini Dodoma Machi 17,2015 kwa ajili ya kufungua rasmi mafunzo ya wakuu wa wilaya wapya yanayofanyika katika ukumbi wa hoteli hiyo
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi mafunzo ya wakuu wa wilaya wapya yanayofanyika katika ukumbi wa hosteli ya St.Gaspar mjini Dodoma Machi 17,2015 Kushoto ni Waziri wa TAMISEMI Mhe.Hawa Ghasia,Watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa na kulia ni Naibu waziri TAMISEMI Mhe.Aggrey Mwanri
Wakuu wa wilaya wakisikiliza kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo kwa wakuu wapya wa wilaya mjini Dodoma Machi 17,2015
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wapya wa wilaya aliowateua hivi karibuni baada ya kufungua semina elekezi ya uongozi mjini Dodoma Machi 17,2015 katika ukumbi wa St.Gaspar Wengine katika picha walioketi mbele ni Waziri wa TAMISEMI Mhe. Hawa Ghasia (Watatu kushoto), Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Aggrey Mwanri (Wapili kulia), Katibu Mkuu TAMISEMI Bwana Jumanne Sagini (kushoto), Mwenyekiti wa wakuu wa mikoa ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro (wapili kushoto), na watano kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa