RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA MRADI WA MAJI LINDI, AWAZAWADIA WASHINDI NANENANE AGOSTI 8,2015

1 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mwakilishi wa shirika la misaada la Ujerumani KFW Bi.Katrin Brandes na mkuu wa mkoa wa Lindi Bibi Mwantum Mahiza wakifunua kitambaa kuzindua ujenzi wa mradi wa maji wa mji wa Lindi eneo la Ng’apa mjini Lindi Agosti 8,2015

2 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima nanenane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi leo.Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuagana na wananchi wa mkoa wa Lindi Agosti 8,2015

3 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja  Jenerali  Raphael Muhuga kombe la ushindi baada ya taasisi anayoiongoza kuibuka mshindi wa taasisi iliyofanya vyema kuliko zote(Overall Best Exhibitor) wakati maonyesho ya sikukuu ya wakulima nanenane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini lindi Agosti 8,2015 5Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Benki ya Maendeleo ya kilimo huko eneo la Ngongo yalikofanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima kitaifa Nanenane Agosti 8,2015

1 Mtaalamu wa Kilimo Dkt.Kissa Kajigili akimpa maelezo ya kilimo bora cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji wa kisasa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipotembelea maonesho ya nane nane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

2 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia muhogo uliolimwa kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo wakati wa maonesho ya kilimo yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima yaliyofanyika kitaifa mkoani humo.  3Mjasiriamali Bi.Ashura Omary Mswazi akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete mafuta ya alizeti aliyokamua kwa mashine bora na kuyauza kupitia kampuni yake ya Kwadelo Investment wakati Rais alipotembea na kukagua baadhi ya mabanda ya maonesho katika viwanja vya Ngongo Mjini Lindi wakati wa sikukuu ya wakulima nanenane

unnamedRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia moja ya matrekta katika viwanja vya maonesho Ngongo Mkoani Lindi wakati wa maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *