Rais Samia Suluhu Hassan afungua Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC)Pemba tarehe 09 Januari, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kikundi cha ngoma ya Kibati ikitumbuiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba kwa ajili ya ziara ya kikazi tarehe 09
Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) Soud Said Ally kuhusu Kituo cha kupimia Karafuu kilichopo katika jengo hilo la Kitega Uchumi la ZSTC Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaabani kuashiria ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) lililopo Chakechake Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaabani pamoja na viongozi mbalimbali wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) lililopo Chakechake Pemba tarehe 09 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Chakechake Pemba mara baada ya kufungua Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) tarehe 09 Januari, 2024.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Immaculate Sware Semesi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Semesi alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu na anachukua nafasi ya Dkt. Samuel Gwamaka Mafwenga ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi huu unaanza tarehe 05 Januari, 2024.