Daily Archives: March 24, 2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA AWAMU YA SABA WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN MARCHI 24,2016

 

3ed23f16-0c44-4473-b466-3e428757aa87Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Zanzibar, Dkt. Mwinyi Haji Makame mara baada ya kuwasili Kisiwani Zanzibar kwa ajili ya sherehe za kuapishwa Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein 

98c2f14d-ba98-49a1-9338-236abf688e95Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kuapishwa kwa Rais wa awamu ya saba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar Marchi 24,

12122Gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na usalama vikiimba wimbo wa Taifa kwenye uwanja wa Amaan

 

 

4cbc1584-f9ea-4af1-9e0c-d9a6da2c13ea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mamia ya wananchi wa Zanzibar mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

93b33dd6-6061-4a53-8fc7-f83698639a97Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimupongeza  Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar.

18d9a0c0-f940-4fcd-b411-bfb73820ac14Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika uwanja wa Amaan kisiwani Zanzibar

3474d22e-c288-4bf8-8049-6e87076866afRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakifatilia kwa makini burudani iliyokuwa ikitolewa na Bendi ya muziki ya Yamoto katika uwanja wa Amaan.

e0a07380-94be-4eba-a31a-a3993af8079eRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jeneral Devis Mwamunyange wakifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na Yamoto bendi katika uwanja wa Amaan.

ff99c854-31e9-4b13-9ebe-3d845a3d56dcRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar

8b05e285-9445-4f7e-ac23-e2a3068a3fca Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika uwanja wa Amaan mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uapisho

TANZANIA NA SAUDI ARABIA ZASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MASUALA YA UCHUMI, BIASHARA, UWEKEZAJI, UFUNDI, VIJANA NA MICHEZO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MARCHI 24,2016

24fe4afc-fd9f-4f7e-9566-6cc3c98559e3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. 

54418b39-66e3-48b7-88d2-11054190b0d3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja, March 24,2016 Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. 

3421f617-7aaf-4396-88c5-eaa3c4fcb8af Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair.

d73e624c-6e46-4e33-97d0-6aaa9d06ad9d Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia kubadilishana hati baada ya uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair

df91a1f9-a99d-4978-892e-efd109efddbf Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Al Jubair, Waziri Mahiga, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kulia) na ujumbe uliombatana na Waziri Al Jubair.