Monthly Archives: August 2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI LEO TAREHE 31 AGOSTI, 2016 AFANYA UTEUZI WA KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

_DSC6220 copy

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Agosti, 2016 amemteua Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Doto M. James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).

Bw. Doto M. James ataapishwa kesho tarehe 01 Septemba, 2016 saa 2:45 Asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile atapangiwa kazi nyingine.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es Salaam

31 Agosti, 2016

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI WA CUBA NA INDIA IKULU DAR ES SALAAM AGOSTI.30, 2016

unnamed-1

 

 

1111hgdgdgdgRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkaribisha na kufanya  mazungumzo na balozi wa Cuba nchini Mhe Jorge Lopez Tormo Ikulu jijini Dar es salaam Agosti 30,2016

1hdgdhghdRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam Agosti 30, 2016