Daily Archives: June 22, 2020

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA IDD HASSAN KIMANTA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kumuapisha Idd Hassan Kimanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Juni 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Idd Hassan Kimanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Juni 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Hassan KImanta akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Laban Kihongosi Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Juni 2020.

Baadhi ya Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wakila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Hassan Kimanta akimuapisha  kamishina msadizi wa polisi Edward Jotharm Balele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Juni 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare akimuapisha Bakari Msulwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Hassan Kimanta watatu kutoka kulia mara baada ya hafla fupi ya uapisho. Wengine katika picha ni Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Laurian Ndumbaro, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. John Pima wakwanza kulia mstari wa mbele, Jerry Mwaga Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wa kwanza kushoto, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa wapili kutoka kushoto, Mkuu wa Wilaya ya Monduli ACP Edward Balele ,wa pili kutoka kulia pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenan kihongosi. Mstari wa Nyuma waliosimama ni Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka pamoja na Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamuhanga.