Monthly Archives: April 2021

MHE RAIS SAMIA ASHIRIKI KIKAO CHA CCM NEC DODOMA LEO

Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshiriki Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ,NEC ambayo yeye ni mjumbe . Mkutano huu umefanyika Makao Makuu ya CCM White House jijini Dodoma, agenda Kuu ikiwa ni kufanya uteuzi wa kujaza nafasi za uongozi ndani ya Chama zilizo wazi kwa sababu mbalimbali, kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama utakaowathibitisha , kesho tarehe 30 April 2021.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM -DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa na Viongozi wengine wakiwa katika kikao cha Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi Kinachoendelea ukumbi wa chama wa Jakaya Kikwete Convetion Center Dodoma leo Tarehe 28 April 2021.