Daily Archives: April 24, 2021

RAIS AFANYA UTEUZI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. John Kedi Mduma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).
Dkt. Mduma ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Uteuzi wa Dkt. Mduma umeanza leo tarehe 24 Aprili, 2021.