Daily Archives: July 5, 2021

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 05Julai, 2021 amemteua Bibi Fatma Ayoub Mwinyimvua Simba kuwa Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU).

Kabla ya uteuzi huo, Bibi Fatma alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMS), Dar es Salaam.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 05 Julai, 2021.