Daily Archives: July 15, 2021

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Apokea Ujumbe Maalum Kutoka Kwa Mfalme Wa Jumuiya Ya Nchi Za Kiarabu (U.A.E) Leo Tarehe 15 Julai, 2021Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Shakhboot Bin Nahyan Al-Nahyan ambaye ni Mjumbe Maalum kutoka kwa Mfalme wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Sheikh Mohammed Bin Zayed Al-Nahyan, mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Barua yenye Ujumbe Maalum kutoka kwa Mfalme wa  Umoja wa Falme za kiarabu (U.A.E) Sheikh Mohammed Bin Zayed Al-Nahyan, uliowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum wa Mfalme huyo Sheikh Shakhboot Bin Nahyan Al-Nahyan ambaye ni Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Shakhboot Bin Nahyan Al-Nahyan, Mjumbe Maalum kutoka kwa Mfalme wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Sheikh Mohammed Bin Zayed Al-Nahyan, Ikulu Jijini Dar es Salaam

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kesho tarehe 16 Julai, 2021 anatarajia kuanza ziara ya Kitaifa ya siku mbili nchini Burundi kwa mwaliko wa Rais Mhe. Evariste Ndayishimiye.

Akiwa nchini humo, Mhe. Rais Samia atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Rais Evariste Ndayishimiye, kisha atashuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari.

Aidha, Mhe. Rais Samia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la Wafanyabishara wa Burundi na Tanzania kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na Burundi.