Daily Archives: July 16, 2021

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Awasili Ikulu Ntare Jijini Bujumbura, Burundi Kuzungumza Na Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Leo Tarehe 16 Julai, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye, alipowasili Ikulu Ntare House Jijini Bujumbura Burundi  katika ziara ya Kitaifa nchini humo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride la Jeshi la Jamhuri ya Burundi  alipowasili Ikulu Ntare Jijini Bujumbura, Burundi  katika ziara ya Kitaifa Nchini humo 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda Mti wa Mwembe mbele ya Jengo la Ikulu ya Ntare Jijini Bujumbura, Burundi  katika ziara ya Kitaifa nchini humo 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu Ntare Jijini Bujumbura

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Awasili Nchini Burundi Kuanza Ziara ya Kitaifa ya Siku Mbili Leo Tarehe 16 Julai, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchion Ndadaye  Jijini Bujumbura Burundi kwa ajili ya kuanza ziara ya kitaifa ya siku mbili nchini humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais wa Burundi Mkuu wa Burundi  Mhe. Prosper Bazombanza alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa Melchion Ndadaye  Jijini Bujumbura Burudi kwa ajili ya kuanza ziara ya kitaifa  ya siku mbili.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alipowasili mjini Bujumbura nchini Burundi.