Monthly Archives: August 2021

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Aanza Rasmi Kurekodi Kipindi Kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini (Royal Tour)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijumuika pamoja na Wananchi mbalimbali katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,2021, alipokua akianza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Msanii Mkongwe wa Taarab Asilia Nchini Bibi Mariam Hamdani, alipokutana nae katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,2021, kabla ya kuanza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Utalii na mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa, wakati wa  kuanza kurekodi rasmi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,2021.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameanza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour chenye lengo la kuitangaza Tanzania kimataifa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya kuratibu Mpango wa kuitangaza Tanzania kimataifa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi, amesema Mhe. Rais Samia atatembelea na kuonesha kwa wageni hao vivutio mbalimbali vya utalii, uwekezaji,  sanaa na utamaduni vilivyopo nchini.

Mhe. Rais Samia na wageni hao wa Royal Tour wameanza zoezi hilo la kurekodi maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii na uwekezaji tarehe 28 Agosti, 2021 katika maeneo ya visiwa vya Zanzibar.