Monthly Archives: September 2021

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 29 Septemba, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Mhe. Tony Blair ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni (Tony Blair Institute for Global Change) amemshukuru  na kumhakikishia Mhe. Rais Samia kuwa taasisi yake inaunga mkono jitahada mbalimbali anazochukua katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.

Amesema ili kuwa na mafanikio ya haraka katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni muhimu kuwa na taarifa sahihi ambazo zitawezesha ufuatiliaji wa karibu wa miradi hiyo.

Kwa upande wake Mhe. Rais Samia amemshukuru Mhe. Tony Blair kwa kukutana nae na kumjulisha ufuatiliaji na uratibu wa masuala yanayofanywa na taasisi yake katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania.

Aidha, Mhe. Rais Samia amesema kwa sasa Serikali inaendelea na utekelezaji wa vipaumbele vyake kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Akutana na Kuzungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu Chamwino Tarehe 29 Septemba, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 29 Septemba, 2021.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana  na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 29 Steptemba, 2021.