Daily Archives: September 6, 2021

Ziara ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Mkoani Manyara na Kilimanjaro Tarehe 05 Septemba, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Mererani Mkoani Manyaara tarehe 05 Sept, 2021 kabla ya kuanza kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini.
Wananchi wa Mererani Mkoani Manyaara wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwasalimia tarehe 05 Sept, 2021 kabla ya kuanza kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Boma Ng`ombe Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro tarehe 05 Sept, 2021 alipokua njiani akielekea Marangu kwa ajili kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasalimia Wananchi wa Himo Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 05 Sept ,2021 alipokua njiani akielekea Marangu kwa ajili kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini
Wananchi wa Himo wakimsikiliza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliposimama kuwasalimia.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema baada ya kukamilika kwa filamu itakayo tangaza utalii, biashara na fursa za uwekezaji nchini kupitia kipindi maarufu cha Royal Tour, dunia itafahamu kuwa madini ya Tanzanite yanachimbwa Tanzania pekee.

Mhe. Rais Samia amesema hayo tarehe 05 Septemba, 2021 wakati akizungumza na wananchi wa Mirerani Mkoani Manyara alipokuwa njiani kuelekea katika mgodi wa Tanzanite.

Amesema filamu hiyo itaweka wazi kwa dunia kuhusu yanapotoka  madini ya  Tanzanite, hatua ambayo itaondoa utata uliopo sasa ambapo baadhi ya mataifa yanadai kuwa ni wazalishaji wa madini hayo.Mhe. Rais Samia amewataka wafanyabiashara kuacha kuuza hovyo madini ya Tanzanite kwani kufanya hivyo kunashusha thamani   ya madini hayo.

Aidha, Mhe. Rais Samia ametembelea eneo la Mlima Kilimanjaro kwa kupitia lango la Marangu, ambapo amesema pamoja na mambo mengine, filamu hiyo ina lengo la kuidhihirishia dunia kwamba Mlima Kilimanjaro upo Tanzania.

Akiwa njiani kuelekea Marangu Mhe. Rais Samia amesalimiana na wananchi wa maeneo ya Boma Ng’ombe na Himo na kuwaahidi kutekeleza ahadi walizoahidi wakati wa kampeni na kutatua changamoto zinazowakabili.