Daily Archives: September 10, 2021

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 10 Septemba, 2021 amemteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Mbunge wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Dkt. Tax ameteuliwa kutoka kwenye nafasi kumi za Wabunge wa kuteuliwa na Rais.

Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Dkt. Tax alikuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye amemaliza muda wake mwezi Agosti, 2021.

Mbunge huyo ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.