Daily Archives: September 18, 2021

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 18 Septemba, 2021 anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo tarehe 23 anatarajiwa kulihutubia Baraza hilo.

Pamoja na Mkutano huo, Mhe. Rais Samia pia atahudhuria  mikutano ya kilele ya kujadili masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)

Aidha, Mhe. Rais Samia anatarajiwa pia kukutana na Wakuu wa Nchi nyingine na viongozi wa Mashirika ya Kimataifa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi na taasisi zao.