Daily Archives: September 20, 2021

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wawili kama ifuatavyo-

  1. Amemteua Bw. Yona Killagane kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO).
  • Amemteua Bw. Mathew Modest Kirama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC).

Kabla ya uteuzi huu Bw. Kirama alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma (DE), Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Bw. Kirama anachukua nafasi ya Bw. Nyakimura Mathias Muhoji ambaye amestaafu.

Uteuzi huo umeanza tarehe 18 Septemba, 2021.