Monthly Archives: October 2021

Mhe. Rais Samia Suluhu hassan Azindua Mwongozo wa Majaji na Mahakimu wanawake na Kupokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Mhe. Rais Yoweri Museven wa Uganda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuzindua rasmi Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 28 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa UN Women hapa Nchini Dkt. Hodan Addou, Balozi wa Sweden Nchini Bw. Anders Sjoberg, Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) Jaji Joaquine De Mello na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante O. Gabriel.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Kitabu cha Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 28 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kushoto Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi, wa pili kushoto Mwakilishi mkazi wa UN Women hapa nchini bibi.  Hodan Addou, kulia Balozi wa Sweden nchini Bw. Anders Sjoberg na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) Jaji Joaquine De Mello.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na Balozi wa Sweden Nchini  Bw. Anders Sjoberg mara baada ya kuzindua rasmi Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Oktoba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Balozi wa Sweden Nchini Bw. Anders Sjoberg, Mwakilishi Mkazi wa UN Women hapa Nchini Dkt. Hodan Addo na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) Jaji Joaquine De Mello baada ya kuzindua rasmi Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia leo tarehe 28 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 28 Oktoba 2021 ameshiriki katika mjadala kuhusu Kipindi cha mpito wa haki wa tabianchi ulioendeshwa kwa njia ya mtandao na Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni, (Tony Blair Institute for Global Change)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, leo tarehe 27 Oktoba, 2021 amewapatia zawadi ya viwanja
wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu ya
Twiga Stars na kuwapongeza kwa kubeba kombe la COSAFA Women’s
Championship nchini Afrika Kusini.
Hafla ya kuwapongeza wachezaji hao, ambayo iliambatana na chakula
cha mchana, imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Baraza la Michezo
Tanzania (BMT).
Aidha, katika hafla hiyo Mhe. Rais Samia amewapongeza washindi sita
(06) wa mashindano ya urembo na utanashati kwa viziwi barani Afrika,
timu za Cricket za wanawake na wanaume kwa kushika nafasi ya tatu
katika mashindano ya Cricket Afrika na timu ya Taifa ya Karate kwa
kutwaa medali nyingi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mhe. Rais Samia amehusisha mafanikio ya timu za Taifa na uwekezaji
ambao Serikali imeanza kuufanya katika kugharamia timu za taifa.
Mhe. Rais Samia amesema alikuwa akiwafuatilia kwa karibu Twiga
Stars wakati wote wa mashindano hayo ya COSAFA na kwamba
amevutiwa na kiwango walichokionyesha kuanzia mchezo wa kwanza
hadi fainali na kuongeza kwamba timu hiyo ya Twiga Stars imeonyesha
ushujaa mkubwa na majina yao yataandikwa katika historia ya michezo
ya nchi yetu.
Vilevile, Mhe. Rais Samia amewaomba mawakala wa wachezaji wa
mpira wa miguu wawasaidie wachezaji wa Twiga Stars ili waweze
kupata nafasi ya kucheza soka la kimataifa nje ya nchi ili kuwainua na
kuisadia timu yetu ya Taifa ya Wanawake iweze kuwa na uzoefu
mchanganyiko, na kuwaasa wachezaji hao kudumisha nidhamu
kwasababu ndio msingi mkuu wa mafanikio.
Sambamba na pongezi hizo kwa Twiga Stars, Mhe. Rais Samia
amempongeza Kocha Mkuu wa timu hiyo Bakari Shime kwa kazi
kubwa aliyoifanya na kuahidi kuangalia namna bora ya kusaidia
kuihudumia Twiga Stars na kutatua changamoto zinazoukabili mchezo
wa mpira wa miguu.
Wakati huohuo, Mhe. Rais Samia amesema mabadiliko aliyoyafanya
hivi karibuni katika muundo wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na
Michezo yalikuwa na lengo la kuleta ufanisi katika masuala ya
utamaduni, sanaa na michezo ili mchango wa sekta hizo katika kukuza
ajira uweze kuonekana.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Samia aliwaombea dua timu ya
Taifa ya Wanawake chini ya Miaka 20 (Tanzanite) ambao wanawania
nafasi ya kucheza Kombe la Dunia mwezi Juni mwakani nchini Costa
Rica.