Daily Archives: October 25, 2021

TAARIFA KWA VYOMBO YA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Mhe. Rais Samia amesema hayo leo tarehe 24 Oktoba, 2021 mara baada ya kuwaapisha viongozi hao katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Amesema uteuzi wa viongozi hao utaleta uwajibikaji mzuri hasa katika sekta ya Habari na Mawasiliano kwasababu hivi sasa inakwenda kwenye mabadiliko ya kukuza matumizi ya teknolojia na kuwataka viongozi hao kuwajibika katika nafasi zao hizo ili Tanzania ipige hatua kimaendeleo.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amewataka viongozi mbalimbali walioteuliwa akitolea mfano Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na kuacha mara moja mivutano isiyo na tija katika majukumu yao.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amempongeza Mhe. Rais Samia kwa jitihada zake anazozifanya na hivi sasa kuna miradi mingi inayotekelezwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ya michezo ambayo hivi sasa inafanya vizuri ndani na nje ya nchi.

Akizungumzia Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali haina wasiwasi nayo kwasababu watendaji wa Tume hiyo wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Aidha, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Akson, amewataka viongozi wa Tume ya Uchaguzi kuwa na utaratibu wakufanya matayarisho ya uchaguzi mapema, badala ya kusubiri hadi uchaguzi unapofika ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wanasiasa dhidi ya Tume hiyo.

Wakati huohuo, Mhe. Rais Samia amewaongoza viongozi mbalimbali kumuaga Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu hapa nchini.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Aagana na Mhe. Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi Uwanja wa Ndege wa JNIA tarehe 24 Oktoba, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 mara baada ya Rais huyo wa Burundi Mhe. Ndayishimiye kuhitimisha zira yake nchini na kurejea Burundi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mke wa Rais Evareste Ndayishimiye wa Burundi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 wakati Mhe. Ndayishimiye alipokua akiondoka kurejea Nchini Burundi baada ya kukamilisha ziara yake leo tarehe 24 Oktoba, 2021. kulia ni Rais wa Ndayishimiye wa Burundi
.
.
.