Daily Archives: November 13, 2021

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 13 Novemba, 2021 amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Adesina Akinumwi.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Akinumwi amempongeza Mhe. Rais Samia kwa jinsi anavyoimarisha sekta binafsi nchini Tanzania kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.

Aidha, Dkt. Akinumwi amemualika Mhe. Rais Samia kuhudhuria Jukwaa La Wawekezaji Afrika, litakalofanyika nchini Abidjan, Côte d’Ivoire mwezi Desemba 2021 ambalo litatoa fursa ya kuwakutanisha na wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kwa upande wake Mhe. Rais Samia amemshukuru Dkt. Adesina Akinumwi kwa mwaliko wenye lengo la kusaidia upatikanaji wa mitaji na uwekezaji wa kimkakati katika miradi ya maendeleo nchini.