Daily Archives: December 4, 2021

Kuelekea Miaka 60 ya Uhuru, Mhe. Rais Samia Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa -Chang’ombe-Sokoine na Kawawa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa katika sherehe zilizofanyika Mbagala Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Wengine katika picha ni Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa katika sherehe zilizofanyika Mbagala Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na viongozi Wengine mara baada ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa katika sherehe zilizofanyika Mbagala Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila wakati akitoa maelezo ya Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa kabla ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Mradi huo.

Sehemu ya Wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa zilizofanyika Mbagala mkoani Dar es Salaam.
.
.

Moja ya Kituo Kikubwa chaMabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) kilichopo Mbagala mkoani Dar es Salaam.

Sehemu ya Barabara ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa mkoani Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mbagala hawaonekani pichani mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa zilizofanyika Mbagala mkoani Dar es Salaam.
.

Kuelekea Miaka 60 ya Uhuru, Mhe. Rais Samia Azindua Rasmi Mradi wa Maboresho ya Miundombinu ya Bandari ya Gati namba 0-7 Bandarini Jijini Dar es Salaam kwa Ajili ya Matumizi leo Tarehe 04 Desemba, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria ufunguzi Rasmi kwa ajili ya matumizi ya mradi wa maboresho ya gati namba 0 hadi 7 katika sherehe zilizofanyika Bandarini Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Eric Hamissi pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kufungua rasmi kwa ajili ya matumizi ya mradi wa maboresho ya gati namba 0 hadi 7 katika sherehe zilizofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Eric Hamissi kuhusu Ujenzi wa gati namba 0 hadi 7 kabla ya kuzindua rasmi kwa ajili ya matumizi katika hafla iliyofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Eric Hamissi pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa kuhusu shughuli mbalimbali za Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kuwasili katika Bandari hiyo ya Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kufungua rasmi kwa ajili ya matumizi Mradi wa maboresho ya gati namba 0 hadi 7 katika sherehe zilizofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021.