Daily Archives: December 6, 2021

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Afungua Barabara ya Moroco Mwenge, awatembelea Mama Maria Nyerere na Mama Anna Mkapa Tarehe 05 Desemba, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Kitambaa kufungua rasmi Awamu ya Pili ya upanuzi wa Barabara ya New  Bagamoyo (Moroco – Mwenge)  Jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 4.3 tarehe 05 Desemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kufungua rasmi Awamu ya Pili ya upanuzi wa Barabara ya New  Bagamoyo (Moroco – Mwenge)  Jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 4.3 tarehe 05 Desemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye Ufunguzi wa Awamu ya Pili ya upanuzi wa Barabara ya New  Bagamoyo (Moroco – Mwenge)  Jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 4.3 tarehe 05 Desemba, 2021.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mama Maria Nyerere wakati alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake Msasani  Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Desemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Kitukuu cha Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wakati alipomtembelea Mama Maria Nyerere kumjulia hali nyumbani kwake Msasani  Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Desemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mama Anna Mkapa wakati alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake Masaki  Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Desemba, 2021.
Wasanii wa Kikundi cha Burudani cha JKT Ruvu wakitoa Burudani wakati wa Ufunguzi wa Awamu ya Pili ya upanuzi wa Barabara ya New  Bagamoyo (Moroco – Mwenge)  Jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 4.3 tarehe 05 Desemba, 2021

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 05 Desemba, 2021 amefungua rasmi Barabara ya New Bagamoyo sehemu ya Morocco hadi Mwenge yenye urefu wa Kilomita 4.3 kwa ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia Shirika lake la Maendeleo la Japani (JICA).

Sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo zilizofanyika Kijitonyama ni sehemu ya Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru ambapo Mhe. Rais Samia anakagua, kuweka Mawe ya Msingi na kufungua baadhi ya Miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jiji la Dar es Salaam.

Mhe. Rais Samia amesema ufunguzi wa barabara hiyo ni juhudi za Serikali katika kuboresha na kujenga miundombinu ya barabara katika Jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kupunguza kero ya msongamano wa magari na ajali za barabarani katika Jiji hilo.

Aidha, Mhe. Rais Samia amewataka wananchi kuzingatia sheria ili kupata manufaa yaliyokusudiwa katika kujenga barabara na miundombinu kwa kuepuka kufanya vitendo vitakavyopelekea uharibifu wa miundombinu hiyo.

Pia, Mhe. Rais ameitaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pamoja na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa barabara na madaraja unafanyika kwa viwango vilivyokubaliwa kimkataba ili zidumu kwa muda uliokusudiwa.

Kuhusu Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Rais Samia amesema kuwa sura ya Jiji imebadilika kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka mitano iliyopita hasa katika miundombinu ya barabara kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) kuwezesha mitaa mingi kuwa na barabara za lami huku akitolea mfano Magomeni na Kinondoni.

Mhe. Rais Samia amesema Serikali inaendelea na kuboresha miundombinu mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kwa sasa inaangalia uwezekano wa kuboresha eneo la Jangwani ambalo limekuwa kero kwa wananchi hususan kipindi cha mvua.

Vilevile, Mhe. Rais Samia amewakumbusha wananchi kuendelea kupata chanjo dhidi ya UVIKO 19 kutokana na tishio la wimbi la nne la ugonjwa huo ambalo limezikumba nchi mbalimbali duniani.

Kuhusu fedha za mkopo wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Mhe. Rais Samia amesema matumizi ya fedha hizo yanahitaji ufuatiliaji makini na kupitia Wizara ya Fedha na Mipango wameanzisha kitengo cha tathmini na ufatiliaji ili kuhakikisha zinafanya kazi iliyokusudiwa.

Wakati huohuo, Mhe. Rais Samia amewatembelea Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere na Mjane wa Hayati Rais Benjamin Mkapa Mama Anna Mkapa, kuwasalimia na kuwajulia hali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru.