Daily Archives: December 10, 2021

Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aondoka Nchini baada ya kukamilisha Ziara yake hapa nchini leo tarehe 10 Desemba, 2021

Mhe.Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 2021 kabla ya kuondoka kurejea nchini Kenya baada ya kukamilisha Ziara ya Kiserikali ya siku moja hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimsindikiza mgeni wake Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 2021 alipokua akiondoka kurejea nchini Kenya baada ya kukamilisha Ziara ya Kiserikali ya siku moja hapa nchini.
Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiagana na baadhi yaViongozi wa Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 2021 alipokua akiondoka kurejea nchini Kenya baada ya kukamilisha Ziara ya Kiserikali ya siku moja hapa nchini. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na mgeni wake Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 2021 alipokua akiondoka kurejea nchini Kenya baada ya kukamilisha Ziara ya Kiserikali ya siku moja hapa nchini.

Mhe. Rais samia Suluhu Hassan na Mhe. Rais Uhuru Kenyatta Wakizungumza na Vyombo vya Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo Rasmi na Ujumbe wa Kenya ulioongozwa na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 2021.
.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu mambo mbalimbali ya Ziara ya Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 2021.
 
.

Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania.