






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao: –
Prof. Othman anachukua nafasi ya Dkt. Fenella Ephraim Mukangara ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Prof. Othman ni Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Dkt. Mlimuka anachukua nafasi ya Prof. Humphrey P.B. Moshi aliyemaliza muda wake. Dkt. Mlimuka ni Mkurugenzi Mstaafu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).
Dkt. Kutua anachukua nafasi ya Dkt. Deudatus Mtasiwa ambaye amemaliza muda wake.
Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Desemba, 2021.