Monthly Archives: January 2022

UTEUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao: –

  1. Amemteua Prof. Ulingeta Mbamba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE).

Prof. Mbamba anachukua nafasi ya Dkt. Ng’wanza Kamata Soko aliyemaliza muda wake.

Prof. Mbamba ni Profesa Mshiriki na Amidi wa Shule Kuu ya Biashara, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  1. Amemteua Bi. Zuhura Sinare Muro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Bi. Muro ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ushauri Elekezi ya Kazi Service Limited na Mkufunzi wa muda katika Taasisi ya Uongozi       (Uongozi Institute), Dar es Salaam.

  1. Amemteua Prof. Leonard James Mselle kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya TEHAMA.

Prof. Mselle ni Mhadhiri, Rasi Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Uteuzi huu unaanza tarehe 29 Januari, 2022.

Mhe. Rai Samia Suluhu Hassan Afanya Ziara ya Kikazi ya Siku Moja Nchini Msumbiji Leo Tarehe 28 Januari, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Philipe Nyusi wa Msumbiji alipowasili katika uwanja wa ndege wa Pemba nchini Msumbiji kwa ajili ya ziara  ya kikazi ya siku moja Nchini humo leo tarehe 28 Januari 2022 Nchini humo.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Mwenyeji wake Rais Philipe Nyusi wa Msumbiji alipowasili  katika uwanja wa ndege wa Pemba nchini Msumbiji kwa ajili ya ziara  ya kikazi ya siku moja Nchini humo leo tarehe 28 Januari 2022 Nchini humo.
.
Rais Philipe Nyusi wa Msumbiji akimtambulisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Msumbiji alipowasili  katika Uwanja wa ndege wa Pemba nchini Msumbiji kwa ajili ya ziara  ya kikazi ya siku moja Nchini humo leo tarehe 28 Januari 2022 Nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Kikundi cha ngoma ya asili ya Msumbiji alipowasili  katika uwanja wa ndege wa Pemba nchini Msumbiji kwa ajili ya ziara  ya kikazi ya siku moja Nchini humo leo tarehe 28 Januari 2022 Nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na  Rais Philipe Nyusi wa Msumbiji alipowasili katika mji wa Pemba Nchini Msumbiji  kwa ajili ya ziara  ya kikazi ya siku moja Nchini humo leo tarehe 28 Januari 2022 Nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na  Vyombo mbalimbali vya Habari Nchini Msumbiji kufuatia ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini humo leo tarehe 28 Januari 2022. Kulia ni Rais Philipe Nyusi wa Msumbiji.
 
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisindikizwa na Mwenyeji wake Rais Philipe Nyusi wa Msumbiji alipokua akiondoka katika Uwanja wa ndege wa Pemba nchini Msumbiji baada ya kukamilisha ziara  yake ya kikazi ya siku moja Nchini humo leo tarehe 28 Januari 2022 Nchini humo.