Daily Archives: January 10, 2022

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Awaapisha Viongozi Wateule Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma Leo Tarehe 10 Januari, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Nape Moses Mnauye (Mb) kuwa Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari leo tarehe 10 Januari, 2022 katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb) kuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb) kuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Hamad Yussuf Masauni kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi leo tarehe 10 Januari, 2022 katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Hussein Mohamed Bashe (Mb) kuwa Waziri Kilimo leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Paschal Katambi Patrobass (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Pindi Hazara Chana (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Khamis Hamza Khamis (Mb) kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Ummy Hamis Nderiananga (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Prof. Eliamani Mathew Sedoyeka kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu Juma Selemani Mkomi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Jaji Jacob Casthom Mwatebela Mwambegele kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Jaji Sam Mpya Rumanyika kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu Patience Kilanga Ntwina kuwa katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora. leo tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma. 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezitaka Wizara zilizogawanywa zianze kujipanga kimuundo na kuanza utekelezaji wa majukumu yake mara moja.

Mhe. Rais Samia amesema hayo leo tarehe 10 Januari, 2022 mara baada ya kuwaapisha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.

Aidha, Mhe. Rais Samia amesema tarehe 13 Januari, 2022 anatarajia kuzungumza na Mawaziri na Naibu Mawaziri walioapishwa Mkoani Dodoma.

Mhe. Rais Samia amesema licha ya kuwaacha katika uteuzi Mawaziri wawili Mhe. Palamagamba Kabudi aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Mhe. William Lukuvi aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ataendelea kuwatumia ili waweze kumsaidia kusimamia viongozi aliowateua kutekeleza majukumu yao.

Hafla hiyo ya Uapisho imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Mhe.Tulia Ackson, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali.