Daily Archives: January 10, 2022

UTEUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 09 Januari, 2022 amemteua Bw. Edward Gerald Nyamanga kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR), upande wa Mazingira.

Bw. Nyamanga anachukua nafasi ya Bw. Esmaily Hassan Rumatila ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Bw. Nyamanga ataapishwa kesho tarehe 10 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.