Daily Archives: January 17, 2022

UTEUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bw. Mcha Hassan Mcha kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mcha alikuwa Kamishna wa Udhibiti na Utekelezaji (Control and Enforcement), Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Bw. Mcha anachukua nafasi ya Bw. Msafiri Lameck Mbibo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Madini.

Uteuzi huu umeanza tarehe 5 Desemba, 2021.

Aidha, Mhe. Rais Samia amemteua Balozi Celestine Joseph Mushy kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria.

Balozi Mushy alikuwa Katibu Tawala Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Uteuzi huu umeanza tarehe 14 Januari, 2022.

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan apokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi wanne Pia Apokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye-Ikulu Chamwino Dodoma tarehe 14 januari, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi uliowasilishwa na Mjumbe maalum ambae pia ni Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni Mhe. Balozi Ezechiel Nibigira, mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 14 Januari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi ambae pia ni Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni Mhe. Balozi Ezechiel Nibigira, mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 14 Januari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Saudi Arabia hapa nchini Mhe. Abdalla Ali M. Alsheryan, leo tarehe 14 Januari 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia hapa nchini Mhe. Abdalla Ali M. Alsheryan, mara baada ya kuwasilisha Hati yake ya Utambulisho leo tarehe 14 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.