Daily Archives: January 21, 2022

Mhe. Rais Samia Suluhu hassan Akisungumza na Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali katika Kikao Kazi Jijini Dodoma tarehe 21 Januari, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali za Serikali katika Kikao Kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete tarehe 21 Januari, 2022 Jijini Dodoma.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Wananchi wa Bomang’ombe Mkoani Kilimanjaro wakati akielekea Moshi mjini tarehe 21 Januari, 2022
 
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tarehe 21 Januari, 2022
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia pamoja na Kikundi cha ngoma za asili ya kabila la Kimasai mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tarehe 21 Januari, 2022

UTEUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kutekeleza majukumu yao kwa lengo la kuwaletea Maendeleo wananchi.

Mhe. Rais Samia ametoa agizo hilo tarehe 21 Januari, 2022 katika Kikao kazi na watendaji hao kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Aidha, Mhe. Rais Samia amewataka Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kufanya kazi kwa kuzingatia Mipango ya kitaifa katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo Dira ya Taifa ya 2020-2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa 2021/22 – 2025/26 na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo inabainisha vipaumbele vya Serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mhe. Rais Samia amewataka viongozi hao kuwa wabunifu na kutekeleza majukumu yao kwa kufuata Sheria, Kanuni na Miongozo ya kiserikali katika kutimiza majukumu yao.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Samia amewasili mkoani Kilimanjaro na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Stephen Kagaigai pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali ambapo kesho tarehe 22 Januari, 2022 atakuwa Mgeni Rasmi katika Tamasha la Utamaduni la mkoa Kilimanjaro.

Akiwa njiani kuelekea Moshi mjini, Mhe. Rais Samia amewasalimia wananchi wa Bomang’ombe, Wilayani Hai na kuwapa pole kwa ukame ulioukumba mkoa huo pamoja na kuwataka kudumisha amani ili Serikali iendelee kuwaletea maendeleo.

Mhe. Rais Samia pia amewahakikishia wananchi hao kuwa Serikali itatatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kero ya maji, vituo vya afya kama alivyofanya katika suala la elimu.