Daily Archives: May 11, 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA KUANZA ZIARA YA KISERIKALI NCHINI UGANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya Ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Uganda kuanzia tarehe 10 – 11 Mei, 2022 kwa mualiko wa Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda.

Hii itakuwa ni Ziara ya kwanza ya Kiserikali ya Rais Samia kufanya nchini Uganda tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie madarakani mwezi Machi 2021.

Madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha na kudumisha zaidi historia iliyopo na mahusiano ya kidiplomasia pamoja na ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili.

Katika ziara hiyo, Wakuu hao wawili wa Nchi na Serikali wanatarajiwa kujadili kuhusu masuala ya nishati, biashara, usafiri, maendeleo ya miundombinu pamoja na sekta za afya.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe Ikulu Jijini Dar es Salaam Tarehe 09 Mei, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo tarehe 09 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe kuhusu mambo mbalimbali ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe mara baada ya mazungumzo yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2022.