Daily Archives: June 1, 2022

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Ahudhuria Tamasha la Dream Concert na Kuzindua Kitabu cha Msanii wa Hiphop Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Serena Jijini Dar es Salaam Tarehe 31 Mei, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wasanii wa muziki wa Hiphop na Bongo flava katika maadhimisho ya miaka 30 ya Msanii Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ya kuwa katika fani hiyo kwenye Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na msanii wa Muziki wRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ukumbi wa Serena pamoja na Msanii wa Muziki wa Hiphop nchini Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na msanii wa Muziki wa Hiphop Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ mara baada ya kuwasili Serena kwa ajili ya kuhudhuria tamasha la maadhimisho ya miaka 30 ya msanii huyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Sasha Joseph Mbilinyi mtoto wa Msanii wa Hiphop Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ katika Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kitabu cha Msanii Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ chenye jina la Muziki na Maisha from the Street katika Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimpa Tuzo Msanii wa Muziki wa Hiphop nchini Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ya kuthamini mchango wake katika Sanaa na kuzalisha ajira kabla ya kuzindua kitabu cha msanii huyo chenye jina la Muziki na Maisha – from the Street to the Parliament  katika Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Apokea Kombe la Dunia Litakalo Shindaniwa katika Mashindano ya Mpira wa Miguu Nchini Qatar, katika Hafla Iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Tarehe 31 Mei, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wadau mbalimbali wa michezo katika hafla ya kupokea Kombe la Dunia litakalo shindaniwa katika Mashindano ya Mpira wa miguu (World Cup) nchini Qatar, iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Kombe la Dunia kutoka kwa Balozi wa Kombe hilo kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil Juliano Belletti katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Balozi wa Kombe la Dunia kutoka (FIFA) mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil Juliano Belletti katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi yenye mfano wa Kombe dogo la Dunia kutoka Balozi wa Kombe hilo kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil Juliano Belletti katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2022.
Wadau mbalimbali wa Michezo pamoja na Viongozi wakiwa kwenye hafla ya mapokezi ya Kombe la Dunia Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2022.
.
.
.\
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akinyanyua juu Kombe la Dunia (World Cup) litakalo shindaniwa katika Mashindano ya Mpira wa miguu yatakayo fanyika nchini Qatar katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2022.