Daily Archives: June 1, 2022

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam Tarehe 30 Mei, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa Profesa Rwekaza Mukandala  aliyeambatana na baadhi ya Wajumbe wa Kikosi kazi hicho Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa Profesa Rwekaza Mukandala kwenye  picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Kikosi kazi hicho mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Mei, 2022.TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA APOKEA KOMBE LA DUNIA (WORLD CUP) JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amepokea Kombe la Dunia (World Cup) litakaloshindaniwa kwenye mashindano ya Mpira wa Miguu nchini Qatar kuanzia 21/11 – 18/12/2022.

Rais Samia amepokea Kombe hilo kutoka kwa Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ambaye ni mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Brazil Juliano Belletti katika hafla iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Pia Rais Samia amesema ujio wa Kombe la Dunia Tanzania utaleta fursa za kiuchumi hivyo kuwataka wananchi kutumia nafasi hiyo kwa manufaa ya taifa.

Aidha, Rais Samia amewataka Watanzania kutumia fursa zinazojitokeza kuitangaza na kuisemea vizuri Tanzania na kuzitumia fursa hizo kibiashara kwa kuuza bidhaa halisi za kitanzania vikiwemo vyakula.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Serikali imeanzisha Mfuko wa Kukuza Vipaji, hivyo kuwataka viongozi kuzitumia vizuri fedha zinazotolewa kwa madhumuni hayo na kuwaandaa vijana kushiriki katika mashindano ya kimataifa.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali, baadhi ya wachezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ akiwemoSunday Manara na Abdallah Kibadeni pamoja na wadau wengine wa michezo nchini.