Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Awasili Zanzibar mara baada ya Kuhitimisha Ziara yake ya Kikazi nchini Oman na Saudi Arabia tarehe 16 Juni, 2022 Leave a reply Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali waliofika kumpokea katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Saudi Arabia mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya Kiserikali nchini Oman, tarehe 16 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Saudi Arabia tarehe 16 Juni, 2022 baada ya kuhitimisha ziara yake ya Kiserikali nchini Oman