Daily Archives: August 1, 2022

Mhe. Rais Samia apokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Comoro Azali Assoumani Ikulu Jijini Dar es Salaam Tarehe 01 Agosti, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Comoro Mhe. Azali Assoumani, ambaye ni Waziri wa Kilimo, Uvuvi, Mazingira, Utalii na Sanaa wa nchi hiyo Mhe. Houmed M’Saidie  mara baada ya kuwasili i Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe, 01 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Comoro Mhe. Azali Assoumani, uliowasilishwa na Mjumbe Maalum ambaye ni Waziri wa Kilimo, Uvuvi, Mazingira, Utalii na Sanaa wa nchi hiyo Mhe. Houmed M’Saidie, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Comoro Mhe. Azali Assoumani, ambae ni Waziri wa Kilimo, Uvuvi, Mazingira, Utalii na Sanaa wa nchi hiyo Mhe. Houmed M’Saidie mara baada ya kuwasilisha Ujumbe kutoka kwa Rais Azali Assoumani Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Picha ya pamoja na Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Comoro Mhe. Azali Assoumani, ambae pia ni Waziri wa Kilimo, Uvuvi, Mazingira, Utalii na Sanaa wa Comoro Mhe. Houmed M’Saidie mara baada mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2022.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na kutengua uteuzi wa Dkt. Raphael Masunga Chegeni.

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Suleiman Mzee alikuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP).

Uapisho utafanyika Ikulu Dar es Salaam, tarehe 1 Agosti, 2022.