Daily Archives: March 19, 2023

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AAHIDI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wanawake kupaza sauti kwa pamoja na kukemea changamoto zinazowakabili wanawake wa Tanzania katika nyanja mbalimbali bila kujali itikadi zao.

Rais Samia ametoa wito huo leo wakati akihutubia katika sherehe ya kilele cha miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, iliyofanyika katika uwanja wa Uhuru.

Aidha, Rais Samia ameahidi kuendelea kutafuta suluhu za changamoto zinazowakabili wanawake na kuwafanya kukosa huduma ikiwemo kujenga shule za wasichana za sayansi na vyuo vya ufundi ili kuwainua wanawake katika masuala ya kiteknolojia.

Kwa upande wa miundombinu, Rais Samia amesema Serikali imeweka bajeti ya kutosha kuiwezesha Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuendeleza miundombinu ya barabara vijijini.

Vile vile, Rais Samia amesema Serikali inaendelea kuimarisha Bandari za Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga, Mtwara na Kigoma ili kuimarisha biashara nchini na ndani ya bara la Afrika kwa ujumla.

Halikadhalika, Rais Samia amesema Serikali itasimamia Tanzania kuwa kinara wa uchumi kwa kumsimamia mwanamke kuzalisha bidhaa mbalimbali zinazouzwa ndani na nje ya nchi kama ilivyopendekezwa na Jukwaa la Usawa wa Kijinsia.

Rais Samia pia ameeleza kuwa changamoto za mabadiliko ya tabia nchi zimesababisha kupanda kwa gharama za bidhaa hivyo, Serikali itaendelea kukabiliana na changamoto hizo kuhakikisha Watanzania wanakuwa na ustawi mzuri wa maisha.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan awaapisha Viongozi Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Tixon Tuyangine Nzunda kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Gerald Msabila Kusaya kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ally Senga Gugu kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Aretas James Lyimo kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.
Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Tixon Tuyangine Nzunda, Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Gerald Msabila Kusaya, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Ally Senga Gugu, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Aretas James Lyimo pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) wakila Kiapo cha Maadili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Tamisemi Anjellah Kairuki, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka pamoja na Makatibu Tawala walioapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.