RAIS KIKWETE ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA MZUMBE, MOROGORO WAKATI WA ZIARA YAKE MOROGORO AGOSTI 25,2O14

1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro baada ya kuwahutubia chuoni hapo Agosti 25, 2014.

2

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika Chuo Kikuuu cha Mzumbe Morogoro baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.

3

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya picha yake ya kuchorwa wakati alipotembelea Chuo Kikuu cha mzumbe ambapo walihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.

4

Meza kuu ikifurahia jambo wakati Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero Mhe Amos Makalla akipohutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.

5

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mhe Boniface Maiga wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.

6

Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mhe Boniface Maiga akisoma risala wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.

7

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua jengo la mihadhara la Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro akisaidiwa na uongozi wa chuo hicho alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.

8

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro wakiweka kumbumbuku ujio wa Rais Kikwete alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.

9

 

TUNAFIKIRIA KUFUTA ADA SEKONDARI – RAIS KIKWETE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza rasmi kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kufuta ada katika shule zake za sekondari, kama namna ya kuboresha Sera ya Elimu na kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anayeanza darasa kwanza anamaliza kidato cha nne.  Rais Kikwete amesema kwamba Serikali yake iliibua mpango wa ujenzi wa sekondari za kata kwa sababu nafasi za wanafunzi kuingia sekondari zilikuwa zimekuwa finyu kiasi cha kwamba ni asilimia kati ya sita na 10 ya watoto wote waliokuwa wanamaliza shule za msingi mwaka 2005 walikuwa wanaingia sekondari wakati anaingia madarakani. Rais Kikwete pia amesema kuwa pamoja na kejeli nyingi zilizoelekezwa kwa shule za sekondari za kata kiasi cha kuitwa Yeboyebo katika miaka ya mwanzoni ya shule hizo, bado zimekuwa na mafanikio makubwa, ambayo ni sehemu ya mafanikio makubwa ya jumla ya Sekta ya Elimu katika miaka karibu tisa ya uongozi wake. Rais Kikwete alikuwa anazungumza jioni ya leo, Jumatano, Agosti 25, 2014, na wanajumuia ya Chuo Kikuu cha Mzumbe cha Morogoro na wakazi wa vijiji vya jirani na chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Morogoro iliyoanza Agosti 20. Katika hotuba yake ya kusisimua, Rais Kikwete ametumia muda wa kutosha kuelezea historia ya maendeleo ya elimu nchini, mabadiliko ya mwelekeo wa elimu na sera ambazo zimeongoza mageuzi makubwa katika elimu chini ya uongozi wake. Rais Kikwete amewaambia mamia kwa mamia ya wanazuoni hao na watumishi wengine wa Chuo hicho pamoja na wanavijiji wa jirani kuwa Serikali wakati wote imekuwa inasaka kubuni sera za kuendeleza elimu nchini na wakati wote kuboresha sera hizo.

“Kwa mfano sasa hivi tunaangalia jinsi gani ya kufuta karo katika shule zetu zote za sekondari za Serikali kama namna ya kuhakikisha kuwa kila mtoto anayeanza darasa la kwanza anakuwa na nafasi ya kumaliza sekondari kwa maana ya kidato cha nne bila kulazimika kuacha shule kwa sababu ya ada,”amesema Rais Kikwete na kuongeza: “Tunaangalia kuondoa ada hii ambako wazazi wanalipa Sh. elfu ishirini kwa shule za kutwa na Sh. elfu sabini kwa shule za bweni, ili watoto wetu waingie darasa la kwanza na kwenda moja kwa moja hadi kidato cha nne bila ya wasiwasi wa kukwamishwa na ada.” 

Akielezea historia ya kuanzishwa kwa Shule za Sekondari za Kata, Rais Kikwete amesema kuwa wakati Serikali yake inaingia madarakani, hali ya watoto kuingia sekondari kutoka shule za msingi ilikuwa mbaya kiasi cha kwamba ni asilimia kati ya sita na 10 iliyokuwa inasonga mbele kwa sababu shule za sekondari zilikuwa chache.

“Kwa miaka mingi, tulikuwa hatukujenga shule mpya za sekondari, na kama mnavyojua wakoloni wa Kiingereza ndio kabisa hawakujenga shule. Kazi hiyo waliwaachia Wamisionari. Kwa hiyo wakati tunaingia madarakani, hali ilikuwa mbaya ndiyo maana tukaja na Sera ya Shule za Kata.” 

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, zilikuwepo jumla ya shule za sekondari 1,745 mwaka 2005 zikiwemo shule 1202 za Serikali na sasa ziko jumla ya shule za sekondari 4,576 zikiwemo shule 3,528 za Serikali. Kuhusu maendeleo ya shule za sekondari za kata, Rais Kikwete amesema kuwa zimekuwa na mafanikio makubwa kama ambavyo Sekta ya Elimu nzima imekuwa na mafanikio makubwa. Rais Kikwete ameelezea baadhi ya mafanikio hayo kama vile upanuzi mkubwa wa elimu ya msingi na uandikishaji wa watoto kuingia shule, upanuzi wa elimu ya sekondari, ongezeko kubwa la wanafunzi wa shule za sekondari, upanuzi wa elimu ya juu ambako sasa kuna vyuo vikuu 51, vikiwemo 15 vya umma, ongezeko la fedha za mikopo ya elimu kutoka sh bilioni 16 mwaka 2005 na kufikia bilioni 345 kwa sasa, kuongezeka kwa wakopaji kutoka wanafunzi 16,000 mwaka 2005 hadi kufikia 95,000 kwa sasa. Rais Kikwete amesema kuwa kwa sasa Serikali yake inapambana na changamoto zilizojitokeza kutokana na kupanuka sana kwa elimu nchini na kuwa moja ya changamoto hizo ni ukosefu wa walimu wa masomo ya sayansi ambapo sasa imefikia kikomo kwa sababu, sasa wapo karibu wa kutosha wa masomo hayo kwa shule za sekondari zote nchini.

 

10

Umati wa wanafunzi, wahadhiri na wananchi wakimsikiliza Rais Kikwete akiwahutubia alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014. 

 

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE WAUNGA MKONO BUNGE MAALUMU LA KATIBA

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe cha Morogoro wameunga mkono mchakato wa Bunge Maalumu la Katiba wakisema kuwa wanaridhishwa na hatua iliyofikiwa na mwendo mzima wa Bunge hilo na kuwa mwafaka unawezekana kuhusu vipengele viliyobakia na kupatikana kwa theluthi mbili za kupitisha Katiba Mpya. Wanafunzi hao wameeleza msimamo wao huo jioni ya leo, Jumatatu, Agosti 25, 2014, chuoni hapo kwenye risala ambayo wameisoma hadharani mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ametembelea chuo hicho ikiwa sehemu ya ziara yake ya siku saba Mkoani Morogoro. Katika risala hiyo iliyosomwa na Rais wa Chama cha Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Bwana Boniface Maige Juma, wanafunzi hao wamesema kuwa ni vyema mchakato huo ukaungwa mkono na kila Mtanzania ili kuuwezesha kuleta neema na matarajio yanayokusudiwa. Amesema Bwana Juma: “Mheshimiwa Rais, tunaridhishwa sana na hatua iliyofikiwa na Bunge Maalum la Katiba. Tunaamini kuwa mwafaka unawezekana kwa vipengele vingine vya Rasimu ya Katiba. Aidha, tunaamini kuwa theluthi mbili za kupitisha Katiba Mpya zinawezekana kupatikana.” Akijibu risala hiyo, Rais Kikwete amewaambia mamia kwa mamia ya wanazuoni, watumishi wengine wa chuo hicho na wanavijiji vya jirani na chuo: “Maoni yenu ndiyo maoni yangu. Ni jambo la kusikitisha kuwa tofauti hizi za viongozi wa siasa zinaleta mfarakano wa namna hii. Tokea mwanzo niliwaambia kuwa wakijiruhusu kushindana na kuviziana katika mchakato huo watakwama.” Ameongeza Rais Kikwete: “Aidha, niliwaambia kuwa Katiba inayotafutwa siyo Katiba ya CCM, ama ya CHADEMA, ama ya NCCR, ama ya CUF. Niliwaambia kuwa hii ni Katiba ya wananchi wa Tanzania. Ni vyema tukakubaliana kuwa yenye kutugawa tukayaacha kwa sasa na kukubali kwa yale ambayo hatuna tofauti.” Kuhusu madai kuwa Rais Kikwete anakataa kukutana na wajumbe wa Bunge hilo ambalo wanaendelea kususia shughuli za Bunge hilo, Rais Kikwete amesema: “Mimi sina tatizo la kukutana nao. Wanajua jinsi ya kukutana nami, ili tuweze kutafuta namna ya kumaliza tofauti hizi.” Hata hivyo, Rais Kikwete ameongeza kuwa ana matumaini kuwa mchakato huu utaweza kuwapatia Watanzania katiba mpya. “Mimi naishi kwa matumaini. Naamini kuwa tutafika mwisho vizuri. Mchakato ni mgumu lakini barabara ndefu haikosi kona. Tukidhamiria kweli kweli tutafika tuendako vizuri.”

MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA MAMA GRACA MACHEL KWENYE OFISI ZA WAMA  AGOSTI 25,2014 .

1

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpokea Mama Graca Machel aliyemtembelea kwenye ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.

2

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Graca Machel wanaonekana wakifurahia jambo kabla ya kupiga picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya WAMA.

3

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni wake Mama Graca Machel na wajumbe wawili wa Bodi ya WAMA. Wajumbe hao ni Mheshimiwa Sophia Simba,Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (kulia) na Mama Hulda Kibacha (wa kwanza kushoto).

4

Mama Garaca Machel akiweka saini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.

5

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA akimkabidhi zawadi ya picha mgeni wake Mama Graca Machel aliyemtembelea ofisini kwake tarehe 25.8.2014.

6

Mkurugenzi wa Idara ya Afya  ya WAMA, Dkt. Sarah Maongezi (kulia) akitoa taarifa ya utendaji kazi wa idara hiyo kwa Mgeni Mama Graca Machel huku Mama Salma Kikwete na wafanyakazi wengine wakisikiliza.

7

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mgeni wake Mama Graca Machel kwenye ofisi za Taasisi hiyo zilizoko karibu na Ikulu.

8

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi baadhi ya majarida yanayochapishwa na Taasisi ya WAMA kwa Mgeni wake Mama Graca Machel.

9

Mama Garaca Machel akimongeza mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete kwa kazi nzuri zinazofanywa na Taasisi yake.

10

Picha ya pamoja kati ya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na wafanyakazi wa Taasissi ya WAMA na Mama Graca Machel na ujumbe wake mara baada ya kufanya mgeni uyo kutembelea ofisi hiyo tarehe 25.8.2014.

11

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwaga Mgeni wake Mama Graca Machel wakati akiondoka kwenye ofisi ya WAMA baada ya viongozi hao kufanya mazungumzo.

12

 

14

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuagana na Mgeni wake Mama Graca Machel nje ya ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *