RAIS KIKWETE AKAGUA CHUO CHA SAYANSI YA AFYA NA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA BINADAMU CHA UDOM OCTOBER 03, 2014

1

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (tai nyekundu) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitivo hicho kianzie kazi rasmi hivi karibuni.2

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali na  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha (mbele) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (kulia) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitivo hicho kianze kazi rasmi hivi karibuni.

3

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo kwa  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (tai nyekundu) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni.  4

Jengo kuu la  Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha Chuo Kikuu cha Dodoma  mjini Dodoma 5

 Sehemu ya majengo ya Chuo  cha Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu ya UDOM mjini Dodoma 6

 Sehemu ya barabara ya lami ya kutoka na kuelekea vyuo mbalimbali vya UDOM7

 Mhe. Baraka Konisaga, ambaye ni Mjumbe wa Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini akitoa hoja binafsi muda mfupi kabla Rais Jakaya Mrisho Kikwete hajafunga rasmi kikao hicho cha siku tatu kilichojumuisha wajumbe zaidi ya 900 kuzungumzia sekta ya elimu ili  kupanga mikakati na kutatua changamoto zinazoikabili, katika ukumbi wa Chimwaga katika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014.  Mhe Konisaga, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, alipendekeza kikao kitoe tamko la pamoja kulipongeza Bunge Maalum la Katiba kwa kuweka historia ya kukamilisha utungaji wa Katiba mpya.

8

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunga rasmi Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini katika ukumbi wa Chimwaga katika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma. 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *