RAIS DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE NA RAIS JOSEPH KABILA WA CONGO WAONGOZA SHEREHE ZA KUHITIMU MAAFISA WAPYA WA JESHI LA JWTZ OKTOBA,18, 2014

1

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maofisa wa Jeshi la ulinzi la JWTZ wanafunzi kundi la 54/13 DRC katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha Oktoba 18, 2014b

 

2

Maafisa wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania wakila kiapo cha utii kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la wananchi wa Tanzania iliyofanyika katika chuo cha mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha Oktoba 18, 2014.

3

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC wakiangalia gwaride katika sherehe ya kuhitimu mafunzo ya maafisa wanafunzi kundi la 54/13 kutoka Tanzania na DRC katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha, (Fuatilia video ya gwaride hilo kwa kubofya hapo chini)

4

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) akimpa zawadi ofisa kadeti Tungohore Yusup kutoka DRC baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika kundi la 54/13 wakati wa hafla ya kumaliza mafunzo iliyofanyika huko Monduli Oktoba,18, 2014.

5

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Rais Joseph Kabila wa DRC akimpa zawadi Ofisa Kadeti Ibrahim Juma Mwamtemi kutoka Jamhuri ya Muungano ya Tanzania baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika mafunzo ya porini wakati wa hafla ya kutunuku kamaisheni baada kumaliza mafunzo ya kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika Chuo cha kijeshi monduli Oktoba,18, 2014.

66

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakijadili jambo wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la 54/13 wa DRC na Tanzania yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha Oktoba 18, 2014

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *